• Breaking News

  Oct 28, 2016

  Serikali Yaanza ‘Kumfilisi’ Sumaye

  HATUA ya Serikali ya Rais John Magufuli kutwaa shamba la Frederick Sumaye, Waziri Mkuu Mstaafu zinaelekea kukamilika, anaandika Pendo Omary.

  William Lukuvi, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi amesema kuwa, hati ya shamba la Sumaye lililopo Bunju, Manispaa ya Kinondoni jijini Dar es Salaam ipo kwenye hatua ya kufutwa.
  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Lukuvi amesema, shamba hilo lipo kwenye hatua ya kufutwa hati yake na kusisitiza, serikali haitavumilia watu wanaomiliki mashamba bila kuyafanyia kazi.

  “Shamba la Sumaye hati yake iko katika hatua za kufutiwa,” amesema Lukuvi na kusisitiza “serikali haitofumbia macho watu wanaomiliki ardhi pia mashamba ambayo hawayaendelezi.”
  Tayari Rehema Mwinuka, Ofisa Ardhi wa wilaya hiyo ameandika barua ya notisi kuelekea kutekeleza kutwaa eneo hilo la Sumaye.

  Hata hivyo, Lukuvi amewataka watu wanaomiliki ardhi kwa kuwa na karatasi za ofa halali, wazibadilishie ili wapewe hati halali.

  Amesema, kuwa kinachoonekana kwa sasa ni kuwa, asilimia 60 ya migogoro ya ardhi, chanzo chake ni karatasi za ofa za halamshauri za jiji na manispaa na kwamba, metoa miezi mitatu kwa wenye karatasi za ofa kubadilishwa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku