Oct 20, 2016

Sharti Jipya: Wanafunzi wasiopanda miti kunyimwa vyeti Iringa

Sharti pekee la mwanafunzi kupata cheti cha kuhitimu elimu ya msingi na sekondari nchini lilikuwa kuhudhuria shuleni, kufanya mitihani na kufaulu, lakini sasa limeongezwa la kupanda miti ambalo halina uhusiano na masomo darasani.
planting-trees

Kuanzia mwakani, moja ya masharti ya mwanafunzi kupewa cheti cha kuhitimu elimu ni kuukabidhi uongozi wa shule mti alioupanda siku ya kwanza alipoanza masomo na akautunza kipindi chote cha masomo.

Sharti hilo lilitangazwa jana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba aliposhiriki mpango wa upandaji miti na wanafunzi katika Shule ya Msingi Mlandege iliyopo Kata ya Kwakilosa, Manispaa ya Iringa akiongozana na viongozi wa mkoa

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR