• Breaking News

  Oct 11, 2016

  Si kweli, Alikiba hakuzinguana na Wizkid – Rockstar4000

  Uongozi wa Rockstar4000 unaomsimamia Alikiba, umekanusha taarifa zilizoandikwa na tovuti maarufu ya Kenya, Nairobi News, kuwa alizinguana na Wizkid wakati wa kuamua nani atangulie kupanda jukwaani kwenye tamasha la Mombasa Rocks, Jumamosi iliyopita.

  Jumatatu hii, tovuti hiyo iliandika habari yenye isemayo: Revealed: The Alikiba-Wizkid Standoff That Almost Ruined Chris Brown’s Mombasa Show.

  Umeandika kuwa Alikiba alikataa kutumbuiza kabla ya Wizkid. “Kiba felt he is bigger in Kenya than Wizkid hence he could not understand why he was scheduled to perform before,” ilikinukuu chanzo kimoja.

  Hata hivyo mmoja wa mameneja wa Alikiba, ameimbia Bongo5 kuwa Wizkid alilazimika kuanza kabla ya Alikiba (tofauti na ilivyokuwa imepangwa) kwa sababu Kiba alikuwa anatumbuiza live na hivyo kurekebisha mitambo ingechukua muda.

  “Wakati ukawa unaenda ikabidi Wizkid aanze sababu yeye alikuwa anaperform semi live,” amesema.

  “Hivyo ikawa ikaamriwa Wizkid aanze. Na Wizkid na Ali hawakuwa na tofauti – infact Wizkid aliposhuka akamwambia ‘Kiba siondoki hapa nataka kuona performance yako.’

  Hata Alikiba kwenye mahojiano maarufu na Willy M Tuva wa Radio Citizen alisisitiza hilo.

  “Nilikuwa mimi naanza kabla ya Wizkid sababu kuna sound pale walikuwa wanaset, unajua live na nanii ilikuwa tofauti so ilibidi jamaa waende wakapige semi live kuokoa muda ili Chris Brown asije akachelewa baadaye,” alisema Kiba.

  Alisisitiza kuwa hakuwa na tatizo la kuanza yeye kabla ya Wizkid.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku