• Breaking News

  Oct 6, 2016

  SIMBA Wampigia Magoti Rais Magufuli....


  Uongozi wa klabu ya Simba SC imemuomba radhi rais magufuli kufuatia kitendo cha kuharibiwa kwa viti kwenye uwanja wa taifa wiki iliyopita wakati wa mechi ya watani wa jadi (K/Koo derby) kati ya Simba na Yanga waliotoka sare ya kufungana bao 1-1.

  Akiongea na waandishi wa habari, msemaji wa timu hiyo Haji Manara amesema Simba inakubali kufanya kosa hilo na kuahidi kuwa kitendo hicho hakitajirudia tena.

  “Rais wa klabu ya Simba, kamati ya utendaji, sekretarieti, benchi la ufundi na wachezaji, wanachama na mashabiki wa Simba wanaomba radhi kwa Rais wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli kupitia kwa waziri mwenye dhamana ya michezo, Nape Nnauye kwa kitendo kisicho cha kiungwana kilichofanywa na mashabiki wetu katika mchezo wa Yanga,” amesema Manara.

  “Tumeona twende mbali na tumwombe radhi rais wetu, hizi ni rasirimali zetu, zinajengwa na kodi zetu, serikali inatumia gharama za kubwa kuziendeleza rasirimali hizi, ni upuuzi wa hali ya juu kabisa kufanyika kitendo kama kile.”

  Aidha Manara ameiomba Serikali iruhusu uwanja huo uendelee kutumika tena na kama inawezekana ifunge kamera za CCTV ili matukio kama hayo ili wahusika waweze kutambulika kiurahisi. Wakati huo huo, kamati ya nidhamu ya TFF imeipiga faini timu hiyo ya shilingi milioni 5 huku ikifuta kadi nyekundu aliyopewa Jonas Mkude wakati wa mchezo huo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku