• Breaking News

  Oct 4, 2016

  Tanzania na Congo zimesainiana mkataba wa makubaliano kutafuta mafuta Ziwa Tanganyika

  ZIARA YA KABILA: Tanzania na Kongo zimesainiana mkataba wa makubaliano kutafuta mafuta Ziwa Tanganyika, Rais Kabila asema mbele ya mwenyeji wake Rais Magufuli Ikulu, Dar.

  Wakati huo huo Rais Magufuli akawataka Wakimbizi wa Congo DRC walioko nchini Tanzania warudi nchini kwao ili wakashiriki kuujenga uchumi wao.

  Pia uchumi wa Tanzania utakuwa kwa asilimia 7.2 kwa mujibu wa takwimu za Benki Kuu (BOT).

  Rais Magufuli: Nimefurahishwa na ziara ya Rais Kabila kwani imelenga kujenga uchumi wa nchi zote mbili na imekuja muda muafaka.

  Rais Magufuli: Tumemkaribisha pia aweke jiwe la msingi katika jengo jipya la Mamlaka ya Bandari ili historia yake izidi kubaki Tanzania.

  Rais Magufuli: Tutaendelea kufanya kazi kwa pamoja, katika kuhakikisha nchi hizi zinajenga uchumi wake kwa pamoja.

  Rais Magufuli: Ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Uganda utarahisisha pia kutoa mafuta kutoka ziwa Tanganyika upande wa DRC hadi Tanga.

  Rais Magufuli: Bandari ya Dar es Salaam imetoa msamaha wa uhifadhi wa mizigo ya DRC bure kutoka siku 14 za awali hadi siku 30.

  Rais Magufuli: Tumezungumza katika suala la biashara kati ya Tz na DRC ilikuwa bilion 23.1, kwa sasa ni bil. 93.6.

  Rais Magufuli: Nimemuomba Rais Kabila awaombe wafanyabiashara wa DCR waje wawekeze Tanzania.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku