Oct 25, 2016

THOMAS Ulimwengu Aipa Mazembe Mkono wa Kwaheri

Thomas Ulimwengu
Mshambuliaji wa kimataifa wa Tanzania, Thomas Ulimwengu ameachana na klabu yake ya TP Mazembe ya nchini Congo DR baada ya kumalizika kwa mkataba wake.

Ulimwengu ambaye ameitumikia Mazembe kwa miaka mitano, ameamua kufatilia ofa mbalimbali za vilabu vya barani Ulaya.

Lich ya TP Mazembe kufanya juhudi za kutaka kumpaka mkataba mpya, Ulimwengu hakuwa tayari badala yake akasisitiza kuwa, ni muda muafaka kwake kufuata nyayo za Mbwana Samatta kwenda kucheza soka la kulipwa bara la Ulaya.

Safasi ya Ulimwengu-TP Mazembe

Ulimwengu alichukuliwa na Mazembe akiwa na miaka 18 akitokea AFC Academy ya Stockholm, Sweden, ameichezea Mazembe jumla ya mechi 130 na kufunga magoli 35 huku akitoa assists za kutosha.

Akiwa na umri wa miaka 23, vilabu vingi vilionesha nia ya kutaka kumsajili, lakini Ulimwengu aliamua kusubiri hadi mkataba wake umalizike ili awe mchezaji huru na kuamua ni wapi ataelekea kuendeleza kipaji chake. Hakuwa tayari kuzungumza na TP Mazembe kwa ajili ya kuongeza mkaba mpya lengo lake likiwa ni kufata nyayo za Mbwana Samatta ambaye kwasasa anatamba na klabu ya Genk nchini Ubelgiji.

Kocha Velud amesikitishwa kwa kuondokewa na mshambuliaji mwenye kasi na nguvu, lakini amesema hamlaumu Ulimwengu kwa uamuzi aliochukua: “Mara zote Thomas amekuwa akicheza kwa kiwango kizuri, ni mchezaji ambaye anafundishika. Namtakia mafanikio kwenye maisha yake ya soka huko aendako.”

“Kabla ya kuondoka Lubumbashi, Thomas Ulimwengu aliacha ujumbe kwa klabu na mashabiki wake: “Kwa kipindi cha miaka mitano, Mazembe imenifanya nikue kwenye maisha ya soka, nawashukuru wote walionisapoti na kushirikiana kushinda mataji tukiongozwa na rais wa klabu Moise Katumbi pamoja na Mrs Carine, viongozi, makocha bila kuwasahaun mashabiki. Ninaamini TPM itashinda taji la CAF. Asanteni wote.”

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR