• Breaking News

  Oct 15, 2016

  Ukiwa na Simu ya Sumsung 7 Marekani Hawezi Panda Ndege Nayo...

  Idara ya uchukuzi nchini Marekani imepiga marufuku simu za Samsung aina ya Galaxy Note 7 kwenye ndege zote nchini humo.

  Hii ni baada ya visa vya simu hizo kushika moto kuripotiwa.

  Abiria hawataruhusiwa kubeba simu hizo ndani ya ndege au hata kwenye mizigo yao wakiingia au kutoka Marekani kuanzia Jumamosi saa 16:00 GMT.

  Idara ya uchukuzi ya Marekani ilikuwa awali imewashauri abriia dhidi ya kuweka simu hizo kwenye mikoba yao.

  Samsung ilitangaza kwamba haitaunda tena simu hizo wiki hii.

  "Tunatambua kwamba kupigwa marufuku kwa simu hizi ndegeni kutatiza baadhi ya abiria, lakini tunazingatia sana usalama wa watu walio ndani ya ndege," karibu wa uchukuzi Anthony Foxx alisema kupitia taarifa.

  Samsung iliwataka watu waliokuwa wamenunua jumla ya simu 2.5 milioni mwezi Septemba kuzirejesha madukani baada ya wateja wengi kulalamika kwamba betri za simu hizo zilikuwa zinalipuka.

  Walipewa simu mpya ambazo zilidaiwa kuwa salama

  Lakini taarifa zilitokea baadaye kwamba hata simu hizo zilizodaiwa kuwa salama zinashika moto.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku