• Breaking News

  Oct 17, 2016

  Unajua Madhara ya Dawa za Kusimamisha Uume Kwa Muda Mrefu?


  Kuna baadhi ya wanaume wanatamani wakati wakiwa wanafanya mapenzi na wenzi au wapenzi wao basi uume zao ziwe zinasimama muda mrefu mathalani masaa matatu au manne au zaidi huku wakimwaga shahawa eti tu wawaridhishe wenzi wao au ili waonekane ni wanaume waliokamilika. Wanaume wengine wamekuwa wakitumia dawa za kusimamisha uume kama vile viagra au dawa za asili na zingine maarufu kama dawa za kimasai! Napenda nikwambie kwamba hizo dawa zina madhara makubwa kwa urijali wako na uko hatarini kuupoteza hata huo urijali mdogo uliosalia!

  Kusimamisha uume kwa muda mrefu na mara nyingine kiasi cha kufikia uume inaanza kuuma kutokana na kusimama muda mrefu tayari ni ugonjwa. Kwa maneno rahisi ni kwamba umetumia dawa za kuongeza nguvu ili kuua nguvu chache ulizokuwa nazo. Kitalaamu hali hiyo ya uume kusimama muda mrefu na kuuma inaitwa 'Priapism'. Priapism hutokea pale uume inapopoteza uwezo wake wa kuondoa damu iliyoko kwenye uume hiyo (ambayo hufanya isimame) ili isinyae (in order to become flaccid). Hiyo hali ikidumu kwa muda wa masaa manne husababisha seli za damu iliyoko kwenye uume kukosa hewa ya oksijeni, hivyo kupelekea tishu katika uume kufa. Na kadri hali hiyo inavyoendelea hupelekea damu kwenye uume kuwa na asidi na hivyo kukosa uwezo wa kusafiri au kutembea kwenda sehemu zingine za mwili hususan kwenye moyo! Hapo hali inakuwa mbaya sana!

  Kuna wanaume wengine wanaji-overdose viagra au madawa ya kienyeji ili wawe wanaume shababi kwelikweli kumbe ndio wanaua uume zao. Ndio maana watu wanaotumia madawa hayo baada ya muda fulani hali zao za kiume zinakuwa mbaya zaidi afadhali ya jana! Ndio maana humu katika blog nimesisitiza sana matumizi ya vyakula na viungo kama tiba ya tatizo la ngivu za kiume! Siwashauri kutumia hayo madawa, otherwise, keep using them for your own risk!

  Bahati mbaya au vyovyote vile kama umesimamisha uumemasaa kadhaa hakikisha katika kipindi cha ndani ya masaa manne tafuta tiba haraka kwa daktari! Wengine baada ya kutumia hayo madawa na uume kusimama kama msumari masaa mengi wao hudhani dawa ni kufanya mapenzi masaa mengi na mwanamke ili kuondokana na hali hiyo! Tena wengine ndo hufurahia eti 'leo mwanamke fulani nitamfaidi kweli...'. My brother you are killing yourself'!!! Hutoweza kumkomoa mwanamke kwa kufanya mapenzi! Matibabu ya tatizo hilo ni kunyonya damu kwa kutumia sindano itakayochomwa kwenye mshipa wa damu uitwayo vein kwenye uume yako! Mwisho nakushauri kula sana vyakula vya asili kama matunda na mboga za majani. Usisahau mazoezi ya viungo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku