Oct 24, 2016

UTATA wa Mamilioni ya Lipumba...Mwenye Adai Anayatoa Mfukoni Kwake


NI shida! Ndivyo unavyoweza kusema baada ya Mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF) anayetambuliwa na Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Ibrahim Lipumba, kuamua kukiendesha chama hicho kwa fedha zake za mfukoni.

Haijajulikana mara moja Profesa Lipumba anakopata fedha hizo, lakini yeye mwenyewe amekuwa akiwaambia watu wake wa karibu kuwa ni malipo yanayotokana na kazi zake za kushauri masuala ya uchumi katika ngazi ya kimataifa.

Taarifa za uhakika na ambazo gazeti hili limezinasa, zinaeleza kuwa hata ziara aliyoifanya hivi karibuni katika baadhi ya mikoa ikiwamo Lindi na Mtwara, imefanikishwa kwa mamilioni ya fedha zilizotoka katika mfuko wa Prof. Lipumba.

Aliporejeshwa tu katika nafasi yake ya uenyekiti na Jaji Francis Mutungi, ambaye ni Msajili wa Vyama vya Siasa nchini, Profesa Lipumba alikaririwa akisema alikuta akaunti ya chama hicho ikiwa haina senti hata moja.

Hata hivyo, alisema suala la fedha ndani ya chama hicho linasimamiwa na Bodi ya Wadhamini wa chama pamoja na Katibu Mkuu, Maalim Seif, ambaye anatambuliwa kama ‘mhasibu mkuu’. Mbali na taarifa hizo, madai mengine yaliibuka hivi karibuni yakimtuhumu Profesa Lipumba kufungua akaunti benki kwa lengo la kuingiziwa fedha za ruzuku, jambo lililopingwa vikali na Baraza la Wadhamini, likisema ni kinyume cha sheria na kwamba mkakati huo una taswira ya kuwavuruga.

Taarifa za sasa za kiongozi huyo kutoa fedha zake mfukoni, zimethibitishwa pia na msaidizi wake wa karibu, Abdul Kambaya, ambaye anashikilia wadhifa wa Naibu Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano wa Umma wa chama hicho.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR