• Breaking News

  Oct 3, 2016

  UTOAJI Hati Viwanja vya Makaburi..Hii Kama siyo Laana, Ni Nini!

  William Lukuvi
  Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi ameagiza kutafutwa kwa maofisa ardhi walioshiriki mchakato wa kutoa hati za viwanja eneo la makaburi lililopo Kinyerezi Sokoni, wilayani Ilala.

  Maofisa hao walitoa hati za viwanja vitatu vya makazi namba 2013, 2015 na 2017 kwenye eneo hilo ambalo waumini wa Kiislamu hutumia kuzikia.

  Akizungumza akiwa eneo hilo juzi, Lukuvi alisema wavamizi hao walikuwa na mpango wa kuhamisha zaidi ya makaburi 500 ili waanze ujenzi.

  Lukuvi alimuagiza kamishna wa ardhi kuwatafuta maofisa wote waliohusika katika mchakato wa kutoa hati hizo popote walipo, ili wachukuliwe hatua za nidhamu na kisheria.

  “Haiwezekani tangu mwaka 1962 watu wanazika eneo hili halafu maofisa ardhi wanawapa watu wengine hati ili wajenge nyumba, nitawashughulikia,” alisema.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku