• Breaking News

  Oct 6, 2016

  VIDEO ya Kusikitisha, Walimu Wakichangia Kumpiga Mwanafunzi Ofisini

  Video hii ambayo imesambaa kwenye mitandao ya kijamii kuanzia leo alfajiri inawaonyesha walimu wakichangia kumpiga mwanafunzi mmoja ndani ya ofisi.

  Walimu hawa wanaonekana si tu wanampiga mwanafunzi huyo kwa viboko, bali wengine wanampiga makofi ya uso, huku walimu wengine wakiwasihi wamuache mwanafunzi huyo kwani wanaweza kumuumiza.

  Haijaweza kufahamika mara moja jina la shule hii, lakini ni ya nchini Tanzania kwani ukutani inaonekana nembo ya serikali. Kwa yeyote anayefahamu anaweza kutuandikia hapa chini ili kuweza kuuhabarisha umma.

  Tazama Hapa Video:

  1 comment:

  1. hawa ni mashetani wala siyo walimu! hivi mzazi wa mtoto huyu kama ataipata video hii si anaweza kuua mtu! Namuomba mwalimu wa kike aliyekuwa anawasihi hao walimu vijana atoe taarifa kwa vyombo husika haraka sana kama anahofu ya mungu, vinginevyo mwisho wa siku wote mlioshuhudia tukio hili la kinyama na mkakaa kimya, mtawajibika na mkono wa sheria. Profesa Joice unashuhudia vijana wako hao? Kama mzazi nina laani kitendo hichi kwa laana zote zilizowahi kutolewa hapa duniani.

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku