Oct 18, 2016

VIDEO:Chanzo Cha Ugomvi wa Godbless Lema na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Gambo Hichi Hapa

Mvutano mkubwa umeibuka kati ya Mkuu wa Mkoa Arusha, Mrisho Gambo na Mbunge wa jimbo la Arusha Mjini, Godbless Lema katika hafla ya uwekaji wa jiwe la msingi katika hospitali ya mama na mtoto inayotarajiwa kujengwa eneo ya Burka eneo lililopo nje kidogo ya jiji la Arusha.

Mvutano huo umeibuka baada ya mkuu wa mkoa wa Arusha kudaiwa kuvuruga ratiba iliyokuwa imepangwa na waandaaji wa hafla hiyo. Kabla ya tukio hilo, inadaiwa kuwa mkuu wa Arusha alikaribishwa na mkuu wa wilaya ya Arumeru Alexernda Mnyeti suala ambalo liliibua mzozo mkubwa kwa wananchi walikuwa wamefika kushuudia tukio la uwekwaji jiwe la msingi.

Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema alisema yeye ndiye aliyetafuta wafadhili na eneo hilo pia ambapo ujenzi huo unafadhiliwa na shirika la kuhudumia afya ya mama na mtoto (Maternity Afrika ).

Inadaiwa kuwa, baada ya mkuu wa mkoa kuanza kuhutubia umma uliokuwa umejitokeza pamoja na wafadhili ndipo Mbunge Godbless Lema aliposimama na kupinga hotuba hiyo kwa madai kuwa imejaa upotoshaji mkubwa kuhusu mradi huo.

Hapa chini ni video za namna tukio zima lilivyotokea;

Mkuu wa Mkoa wa Arusha =, Mrisho Gambo akitolea ufafanuzi juu ya mradi huo wa ujenzi wa hospitali,
Mbunge wa Arusha Mjini, Gobless Lema akizungumza kuhusu mradi huo wa ujenzi wa hospitali


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR