• Breaking News

  Oct 5, 2016

  VITA vya Syria na Hatari ya Kuzuka Vita vya Tatu vya Dunia

  VITA vinavyoendelea nchini Syria vilivyodumu kwa miaka mitano sasa viko mbioni kuiingiza dunia yetu katika Vita Vikuu vya Tatu vya Dunia. Wakubwa wa Dunia yetu, Marekani na Urusi, wanaonekana kutofautiana kwa kiasi kikubwa ambapo sasa Marekani anasema hataki tena mazungumzo na mwenziwe Urusi kuhusu suluhisho la mgogoro wa Syria kwa njia ya amani bali anaangalia "Njia Mbadala" ya kumaliza mgogoro huo. Je, njia hiyo ni ipi?

  Urusi yeye anadai yupo nchini Syria kwa mwaliko wa Rais Bashar Al Assad ili kumsaidia kupambana na makundi ya kigaidi yanayotishia utawala wake. Marekani kwa upande wake anaunga mkono kundi linalojiita Free Syrian Army kwa lengo la kumng'oa Rais Bashar Al Assad madarakani, ingawa wachambuzi wa mambo wanadai makundi yote ya kigaidi yanayopigana nchini Syria dhidi ya serikali ya Rais Bashar Al Assad, likiwemo kundi la Al Qaeda, yaliundwa na yanafadhiliwa na Marekani na nchini nyingine za Magharibi.

  Urusi tayari ina zana za kutosha nchini Syria yakiwemo makombora yake ya kujihami ya S-400 kwa ajili ya kulinda anga. Vivyo hivyo Marekani nayo inadaiwa kupeleka silaha nchini Syria kupitia kwa makundi ya kigaidi.

  Mapigano makali kwa sasa yanaripotiwa jijini Aleppo kati ya majeshi ya Assad na yale ya kigaidi, wote wakigombea umiliki wa mji huo.

  Je, kivipi mgogoro huo unaweza kugeuka vita vya dunia? Kutokana na wakubwa hawa wawili Marekani na Urusi kuwa na masilahi yanayokinzana katika ardhi ya Syria yanayohusisha matumizi ya silaha, upo uwezekano mkubwa wa mgogoro huo kuwa wa dunia nzima. Hivi sasa Vladimir Putin anaonekana kuutawala uwanja wa mapigano nchini Syria kitendo ambacho Marekani hawatakubali kuona wakishindwa na kuaibishwa! Watakapoamua kuingilia kati moja kwa moja kwa kutuma askari wake na silaha zake, hapo ndipo patakuwa patamu maana Urusi naye hatakuwa na njia nyingine bali kuingia kimoja Syria na ikizingatiwa kwamba Urusi wana "ka historia ka kushinda vita japo kwa mbinde"; mfano, mwaka 1812 waliwanyuka Ufaransa na wakati wa WWII (1939 - 1945) tena wakawanyuka Wajeremani wa Hitler.

  Kama inavyofahamika, Marekani ni mjumbe wa NATO, hivyo kuingia kwa marekani nchini Syria kupigana, kutamaanisha kundi la NATO kuingia vitani. Kwa upande wake Urusi, naye anao washirika wake kama China na Iran na wengine. Ikifikia hatua hiyo, nchi kama Korea ya Kaskazini inaweza kutumia mwanya huo kushambulia masilahi ya Marekani popote pale itakapoona panafaa.

  Pale Mashariki ya Kati penyewe hapaeleweki hata kidogo -- Marekani iko na Israel na Saudi Arabia; Urusi ndiyo hivyo tena iko na Iran, Syria yenyewe, na Uturuki kwa mbali japo nayo ni ndumilakuwili.

  Cha kutisha zaidi kuhusu wakubwa hawa kuingia vitani, ni silaha za kisasa na hatari zaidi, zikiwemo za Nyuklia wanazozimiliki, ambazo wakiamua kuzitumia basi ni majanga tupu.

  TUOMBE TU HAWA WAKUBWA WAELEWANE ILI KUEPUSHA ZAHAMA HII
  Imeandaliwa na:
  Pasaka Osunga Rucho
  0756231744.
  Mwalimu anayesubiria ajira.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku