• Breaking News

  Oct 6, 2016

  VITUO Binafsi vya Afya Vinara Utoaji Mimba

  Baadhi ya vituo vya afya vinavyomilikiwa na watu binafsi vinadaiwa kutumika kutoa mimba badala ya kufanya kazi iliyokusudiwa.

  Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru, George Mbijima amesema hayo wakati akifungua kituo cha afya cha Kwema katika Kata ya Nyasubi, Halmashauri ya Mji wa Kahama.

   Amesema kumtoa mtu mimba ni kosa la jinai, yeyote au kituo kitakachobainika kufanya uozo huo, Serikali haitasita kuchukua hatua ikiwa ni pamoja na kukifungia.

  Kiongozi huyo amesema malengo ya Serikali kutoa vibali kwa watu binafsi ni kutaka kusaidia huduma za afya kwa wananchi ziwafikie kwa karibu, lakini wengine wamekuwa wakivitumia vituo hivyo tofauti na malengo.

  Mbijima amewataka pia wamiliki wote wa sekta binafsi kuajiri watumishi kwa kufuata misingi ya sheria na wahakikishe wanalipa kodi stahiki inayolingana na shughuli wanazozifanya.

  Mkurugenzi wa Kituo cha Afya cha Kwema, Pauline Mathayo amesema kituo hicho kitahudumia zaidi ya wakazi 20,000 wanaozunguka kata hiyo.

   Mathayo amesema mpaka kukamilika kwa kituo hicho, ujenzi wake umegharimu Sh578 milioni.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku