Oct 12, 2016

WABUNGE wa CUF Wakamatwa na Polisi Usiku Huu

Baada ya "Bwana Yule" kumaliza ziara yake katika baadhi ya wilaya za Kusini mwa Tanzania huku akilindwa na Polisi, Polisi hao hao jioni hii wamewakamata wabunge wa CUF, Mhe. Bungala (BWEGE) wa Kilwa na Mhe. Katani Katani (Mbunge wa Tandahimba) wakiwa wanakula chakula kwenye mgahawa. Tukio hili limetokea wilayani Nachingwea.

Lengo la Polisi ni kuwazuia viongozi hao wasiendelee na ziara ya vikao vya ndani kama ilivyokuwa kwa "Bwana Yule". Yaani kwa maneno mengine, dola inataka BWANA YULE afanye ziara za kuivunjavunja CUF huku viongozi wa CUF wakizuiwa kukilinda chama. Nimewahi kusema huku nyuma kuwa mwisho wa mapambano haya wapo watu watajulikana kwa rangi zao, sura zao na kazi zao. CUF itashinda mapambano haya.

Mtatiro J

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR