Oct 18, 2016

Wadau wa Elimu Wamgeuzia Kibao Joseph Mungai

Siku moja baada ya aliyekuwa Waziri wa Elimu katika Awamu ya Tatu, Joseph Mungai kusema hakuvuruga mfumo wa elimu katika uongozi wake, wadau wa sekta hiyo wamepinga wakisema  umevurugwa na mawaziri kwa kutofuata Sheria ya Elimu ya mwaka 1979 na kujiamulia mambo.

Mungai ambaye alikuwa akijibu tuhuma zilizoelekezwa kwake baada ya kustaafu siasa alisema Rais wa Awamu ya Nne, Jakaya Kikwete hakumteua kuendelea kuongoza elimu kwa kuwa alitaka kufurahisha walimu waliokuwa wakimchukia kutokana na kuwabana.

Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT), Ezekiah Oluochi alisema mawaziri waliopita na aliyepo sasa wamenchangia kushuka kwa kiwango cha elimu kwa asilimia 90 kwa kutofuata sheria ya elimu.
Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR