• Breaking News

  Oct 16, 2016

  Wadau Waanza Kuhoji Elimu ya Mbowe..Wadai Aonyeshe Cheti Chake cha Form Four

  By Lizaboni
  Nianze kwa kusema kuwa lengo la chama chochote cha siasa ni kutwaa dola. Chama cha siasa si kama chama cha Mpira wa miguu ama chama cha kuimba muziki wa singeli. Kwa maana nyingine chama kinachoshinda uchaguzi ndicho hutwaa mamlaka ya nchi na ndicho huunda Serikali. Ni kwa muktadha huo, Kiongozi wa Chama cha Siasa anapaswa kuwa na sifa zile zile ambazo kiongozi wa nchi anapaswa kuwa nazo. Hata kama Mwenyekiti wa chama kilichoshinda hajagombea, ataendelea kuwa mwenyekiti wa chama hicho na atasimamia utendaji wa Rais wake.

  Hii ni hoja ya msingi sana na sijajua kwa nini wasomi wengi bungeni akina Tundu Lissu hawalioni? Sijajua pia kwa nini washirika wa ukawa akina James Mbatia hawalizungumzi kwa lengo la kutoa hoja ili lijadiliwe bungeni.

  Wadau, chaka kikiongozwa na kihiyo madhara yake ni makubwa. Chama kinakuwa cha hovyo na kinakuwa na watu wa hovyo. Ndo maana hata kwenye uchaguzi wanafanya hovyo. Kwani Mwenyekiti hovyo huzaa chama hovyo na wafuasi hovyo.

  Tuache masihara katika masuala ya nchi. Hivi mliwahi kujiuliza kwa sasa kwa nini Mbowe hana hamu ya kugombea Urais? Anatamani sana tena sana ila vigezo na masharti havikidhi. Ni Form Four Leaver! Nasikia hata hicho cheti cha form four alikipata kimagumashi. Ndio maana humsikii anasema lolote kuhusu vyeti feki kwa vile hata yeye ana cheti feki cha kidato cha Nne.

  Taarifa zilizopo ni kwamba, Freeman Mbowe hakuwahi kufanya na kufaulu mtihani wa Kidato Cha Nne lakini ana cheti cha Form Four. Hakuna ushahidi na wala uthibitisho kuwa alifanya mtihani huo. Je Mbowe alipataje cheti cha Form Four wakati hajawahi kufanya na kufaulu mtihani huo? Nini kilichopo nyuma ya pazia? Nani alisimamia hilo?

  My brother Freeman Aikael Mbowe, ili kuondoa shaka hiyo kuwa hujafanya na kufaulu mtihani wa kidato cha Nne, hebu jitokeze hapa au wape wale vijana wako waiweke hapa kuondoa huo utata. Kuendelea kukaa kimya ni sawa na kuhalalisha kuwa kisemwacho kipo.

  Katika kurahisisha utetezi wako, hebu jibu maswali haya.

  1. Je ulianza kidato cha kwanza mwaka gani na ulimaliza lini?
  2. Ulisoma shule gani?
  3. Wakati unamaliza kidato cha Nne, Mkuu wako wa Shule alikuwa anaitwa nani?
  4. Unakumbuka namba yako ya usajili wa mtihani wa Form Four? Itaje.
  5. Matokeo ya Form Four yalikuwaje? Je yalikuwezesha kuendelea na elimu ya kidato cha Tano?
  6. Ambatanisha vielelezo ikiwa ni pamoja na nakala ya Cheti cha Kidato cha Nne

  By Lizaboni/Jamii Forums

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku