• Breaking News

  Oct 18, 2016

  Wajeruhiwa kwa Bomu Wakimkamata Mtuhumiwa

  Polisi na raia wanne wamejeruhiwa kwa bomu la kutupwa kwa mkono walipokuwa wakimkamata mtuhumiwa wa ujambazi kwenye Kijiji cha Uvinza mkoani Kigoma.

  Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kigoma, Ferdinand Mtui alisema jana kuwa tukio hilo lilitokea Oktoba 14.

  Mtui aliwataja majeruhi hao kuwa ni askari polisi F.3187 Koplo Isaya na raia Saidi Mohamed, Seleman Kashali, Joseph Daudi na Hassan Nasibu, wote wakazi wa Kijiji cha Uvinza.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku