• Breaking News

  Oct 9, 2016

  Waliotimuliwa Udom wakibeba chuo Moro

  Baada ya kukaa miaka zaidi ya 50 bila ukarabati, hatimaye Chuo cha Ualimu Morogoro kimeanza kukarabatiwa ili kipokee wanafunzi 1,138 walioondolea Chuo Kikuu cha Dodoma (Udom).

  Ukarabati huo unaofanywa chini ya ufadhili wa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi utagharimu Sh700 milioni.

  Mkuu wa chuo hicho, Augustine Sahili amesema huo ni mpango wa Serikali unaohusisha vyuo vyote vya ualimu ambavyo vitapokea wanafunzi walioondolewa Udom kutokana na kutokuwa na sifa za kujiunga na chuo kikuu.

  Amesema ukarabati huo utakaomalizika mwezi huu unahusisha mabweni, madarasa na mfumo wa majitaka.

  Pia, ameishukuru Serikali kwa kuona umuhimu wa kukarabati chuo hicho kwani tangu kilipoanzishwa mwaka 1926 hakijawahi kufanyiwa ukarabati mkubwa.

  Mwalimu Anna Mushi aliyehitimu chuoni hapo, amesema majengo mengi na miundombinu vilikuwa chakavu.

  “Vyuo vingi vya ualimu vya Serikali vilianza kabla ya Uhuru, hivyo vinahitaji ukarabati ili viendelee kuwa katika hali nzuri,” amesema mwalimu huyo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku