• Breaking News

  Oct 31, 2016

  Wamachinga Barabara za Mwendo Kasi Kukiona Cha Moto Ilala Kuanzia Kesho

  Halmashauri ya manispaa ya Ilala jijini DSM kesho inaanza rasmi Operesheni ya kuwaondoa wafanyabiashara wote wanaoendesha biashara kando ya barabara za mwendo kasi kuanzia eneo la Gerezani Kariakoo hadi Fery Kivukoni kwa kuwa kufanya hivyo ni kwenda kinyume cha sheria mbali ya kusababisha usumbufu na ajali kwa watembea kwa miguu.

  Mkuu wa wilaya ya Ilala Sofia Mjema akizungumza na waandishi wa habari amesema zoezi hilo litaanza mapema asubuhi na kuwataka wafanyabiashara hao kwenda katika maeneo waliyopangiwa ikiwemo soko Mburahati, Kigogo Sambusa na maeneo rasmi yaliyoainishwa.

  Katika eneo la kariakoo chanel ten imeshuhudia adha kubwa kwa wananchi wanaotembea kwa miguu ambapo wanalazimika kupita katikati ya barabara ya magari ya mwendo wa haraka huku magari hayo yakipita kwa kasi na kuhatarisha maisha yao kutokana na wafanyabiashara hao kupanga biashara zao katika njia za watu wanaotembea kwa miguu.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku