• Breaking News

  Oct 17, 2016

  Wanafunzi UDSM Walalamikia Vigezo Vipya Vya Utoaji wa Mikopo

  Baadhi ya wanafunzi wanaosoma chuo kikuu cha Dar es salaam wameilalamikia serikali kupitia wizara ya Elimu kubadili vigezo vya utoaji wa mikopo bila taarifa jambo lililowasababishia usumbufu mkubwa wanafunzi waliofika chuoni hapo huku wakikabiliwa na maisha magumu baada ya kukosa fedha za kujikimu pamoja na malazi.

  Mwisho mwa wiki wizara ya elimu ilitangaza majina ya wanafunzi watakaopata mikopo pamoja na vigezo vilivyotumika ikiwemo wanafunzi waliosoma masomo ya sayansi, wenye ufaulu wa juu na walemavu na yatima pamoja na ufaulu wa waombaji katika ameneo ya vipaumbele na umahiri huku vigezo hivyo vikiwaacha nje asilimia kubwa ya wanafunzi ambao wanachukua masomo sanaa.
  Wakizungumzia adha hiyo wanafunzi hao wamesema hakuna aliyetarajia kutokea kwa hali hiyo kwani hawakutangaziwa mapema kwamba utaratibu wa utoaji wa mikopo umebadilika hivyo wazazi nao wazazi wamewasafirisha watoto wao kutoka mikoani wakitegemea udhamini kutoka bodi ya mikopo ambayo hata hivyo haijulikani ni lini itatolewa huku wakilandalanda mitaani bil kufahamu hatma yao.

  Charles Kayoka ni mhadhiri wa chuo kikuu cha Dar es salaam ambaye anazungumzia mabadiliko hayo kuwa kutokuwepo kwa sera ya ya elimu ya kudumu ni moja ya sababu ambazo zinaifanya serikali kubadilisha taratibu zake kulingana na nyakati lakini pia ameikumbusha serikali kuwa haitaweza kufanikiwa katika utelekezaji wa kauli mbiu ya tanzania ya viwanda bila ya kuwepo na wataalamu waliosomea sanaa

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku