• Breaking News

  Oct 16, 2016

  Wananchi Wajichukulia Sheria Mkononi Waua Mtu Mmoja Aliyedaiwa Kuwa Ni Panya Road Mbagala Jijini Dar Es Salaam

  WANANCHI wa Mbagala sabasaba wamemuua kwa kumshambulia kwa mawe na kisha kumchoma moto kijana mmoja anayedaiwa kuwa ni mharifu wa kundi la panya road ambaye alikuwa na wenzake zaidi ya 15 ambapo wawili kati yao walipoteza fahamu kutokana na shambulio hilo.

  Tukio hilo la kushambuliwa kwa panya road hao lilitokea majira ya saa 11 jioni katika eneo la Mbagala Sabasaba baada ya vijana hao kukurupushwa walipokuwa wakikimbia walipokuwa wakifanya uhalifu maeneo ya sabasaba Magengeni na Mbagala Zakhem.

  Polisi waliofika eneo la tukio walilazimika kutumia risasi za moto kuwatawanya wananchi ili waweze kuuchukua mwili wa kijana huyo ambaye hakufahamika jina lake.

  Akizungumza na mtandao wa www.habari za jamii.com mmoja wa watu walioshuhudia tukio hilo ambaye alijitambulisha kwa jina moja la Khalfan alisema usalama wa wananchi upo mashakani kufuatia kundi hilo la panya road.

  "Hawa panya road walikuwa zaidi ya 15 wakitokea Mbagala Zakhem ambako walikuwa wakikimbizwa na wananchi baada ya kufanya uhalifu na walipofika hapa Sabasaba walizingirwa na wananchi ambapo watatu kati yao walianza kushambuliwa na mmoja kupoteza maisha baada ya kuchomwa moto " alisema.

  Wananchi wakiangalia mwili wa kijana anayedaiwa kuwa ni wa kundi la kihalifu la panya road aliyeuawa baada ya kufanya uhalifu maeneo ya Mbagala Zakhem Dar es Salaam leo jioni. Katika tukio hilo vijana wengine wawili walipoteza fahamu kutokana na kipigo cha wananchi.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku