Oct 23, 2016

WASTAAFU 30 Watapeliwa Mafao Yao Dodoma..Tahadhari Yatolewa

Walimu wastaafu nchini wametakiwa kuchukua tahadhari ya kuepuka kutapeliwa mafao yao kupitia mitandao ya kifedha na wajanja walioibuka baada ya wastaafu zaidi ya 30 wilayani Kondoa mkoani Dodoma kutapeliwa mafao ya kiinua mgongo,sambamba na kupotea kwa faida katika mazingira ya kutatanisha baada ya kuweka mafao yao kwenye taasisi za fedha ili kupata faida.Tokeo la picha la fedha

Tahadhari hiyo imetolewa na Afisa Utumishi wa CWT-taifa,Bw Ali Shabani kwa niaba ya Katibu wa CWT-taifa Bw Yahaya Msulwa wakati wa uzinduzi wa ujenzi wa Ofisi ya Chama hicho ya wilaya pamoja na kuwakabidhi mabati 360 walimu 36 waliostaafu mwaka huu ili kukabiliana na maisha yasiyotegemea ujira,huku akidai kwamba kutokana na kufikishwa kwa malalamiko hayo ya utapeli kwenye vyombo vya dola lazima wastaafu kuwa makini.

Awali akitoa taarifa ya wilaya ya Kondoa,Katibu wa CWT Bw Darabe amesema licha ya walimu kudai deni la zaidi ya shilingi Mil.335 lakini pia walimu 718 waliopandishwa madaraja kwa mwaka 2016/17 wanalalamikia kunyang’anywa kwa madaraja yao,huku Afisa Utumishi wa halmashauri ya mji wa Kondoa bw Pepino Mfugale akikanusha madai hayo.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR