• Breaking News

  Oct 11, 2016

  Waziri Angela Kairuki Adai Baada ya Kuhakiki vyeti Atahikiki Pensheni Kwa Wastaafu Serikalini

  Waziri wa utumishi wa umma mh. Angella Kairuki amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi la uhakiki wa watumishi hewa na vyeti feki, serikali itaanza jukumu la kuhakiki watumishi wastaafu serikalini nchi nzima ili kujilidhisha malipo yao.

  Alisema kuwa zoezi hilo limeanzia mkoa wa Pwani kwa ratiba ya awali na ameahidi kutoa ratiba kwa mikoa mingine kwa nchi.

  Amewataka wastaafu wote kujitokeza kwa ajili ya zoezi hilo.

  My take: Kuna vijana serikali iliwaajiri mwezi wa tano mwaka 2016, baada ya kuwasainisha mikataba na kuanza kazi serikali ilisimamisha ajira zao kwa muda usiojulikana katikati ya mwezi wa sita mwaka 2016 mpaka sasa vijana hao wapo nyumbani hawajui hatima yao nini na serikali ipo kimya.

  Familia zao zinapata shida ziwasaidieje maana kabla hawajaaliwa na serikali walikuwa wanafanya kazi sector binafsi baada ya serikali kuwaita kazini waliacha kazi sector binafsi na kuja kulitumikia taifa lao, sasa hivi serikali imewatelekeza vijana hawa walioajiriwa kada za afya ,mikoani,wilayani,mahakama nk

  Naomba viongozi wa serikali kulifanyia kazi, pia nawaomba tume za wafanyakazi zilifanyie kazi hili

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku