• Breaking News

  Oct 6, 2016

  Wizara ya ujenzi kupima ufanisi wa watumishi walioko kwenye idara na taasisi zilizoko chini yake.


  Wizara ya ujenzi uchukuzi na mawasiliano inaandaa mpango wa kupima ufanisi wa watumishi wote walioko kwenye idara na taasisi ili kuboresha utendaji kazi wa watumishi na kuondoa wanaofanya kazi kwa mazoea ikiwa ni mkakati wa kuboresha ufanisi katika utoaji huduma kwa jamii.

  Waziri wa ujenzi uchukuzi na mawasiliano Profesa Makame Mbarawa anabainisha mpango huo wa wizara katika kikao kati yake na wataalam kutoka wakala wa barabara nchini Tanroads kulichojadili na kuweka mikakati ya uimarishaji wa kazi na umuhimu wa utawala bora katika sehemu zao za kazi kwa lengo la kuleta mabadiliko.

  Katika kikao hicho waziri Mbarawa akadokezewa kuwa sekta ya ujenzi inakabiliwa na changamoto ya upungufu wa wataalam waliobobea na wachache waliopo tayari umri umeshawatupa mkono ambapo ameagiza aletewe orodha ya mahitaji ili aweze kutangaza nafasi za ajira huku kipaumbele kikitajwa kuwa ni vijana.

  Kwa upande wake mtendaji mkuu wa wakala wa barabara Tanroads Mhandisi Patrick Mfugale amesema licha ya mafanikio makubwa waliyopata wakala hao lakini bado kubwa changamoto kadhaa ambazo zinahitaji kufanyiwa kazi ikiwemo suala la uzito kupitiliza wa magari ya mizigo ambayo huaribu barabara kwa kiasi kikubwa.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku