• Breaking News

  Nov 12, 2016

  Ali Kiba Awatolea ‘Povu’ Wanaomtukana Wizkid Mitandaoni Kuhusu MTV EMA

  IKIWA ni baada ya waandaaji waTuzo za MTV EMA 2016 kumpokonya tuzo ya Best African Act mwanamuziki wa Nigeria, Wizkid na kuahidi kumkabidhi Mbongo Fleva, Ali Kiba, kumekuwa na minonong’o mingi na comment mbaya za mashabiki mitandaoni wakimshambulia kwa matusi na kejeli Wizkid aliyepewa tuzo hiyo kimakosa.

  Hali hiyo imemfanya Alikiba afunguke na kuelezea namna anavyokerwa na baadhi ya watu wanavyomshambulia Wizkid ilihali wao Kiba na staa huyo wote ni wanamuziki na hawajawahi kugombana.

  Kiba hakukomea hapo, alienda mbali zaidi kwa kupost picha ya aliyopiga akiwa na Wizkid na kuandika maneno haya kwenye akaunti yake ya Instagram.

  “Sijafurahishwa na ninachokiona kinaendelea kwenye mitandao ya kijamii, ninamkubali sana wizkid kama msanii mwenzangu na kama mshabiki pia. Nimesikitishwa sana na kushtushwa kuona watu wakimdhihaki Wizkid kwa maneno yasiofaa na matusi, nataka kuwa muwazi tu naamini kuwa haya maneno yakijinga na yasiyofaa hayahusishi na hayajatoka kwa mashabiki wangu wa kweli kwasababu nafahamu wamekuwa wakijua jinsi gani namkubali Wizkid.

  usizamishwe na maneno ya mahater bro, hongera sana kwa kuwa mwaka huu umekuwa wa mafanikio kwako, upendo wa dhati kutoka kwa mashabiki wangu wa kweli na nchi ya Tanzania pamoja#KingKiba,” Ameandika Kiba.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku