• Breaking News

  Nov 12, 2016

  Alichokiandika Donald Trump Kuhusu Walioandamana Kisa Kashinda

  Wamarekani wengi wameingia barabarani na kupiga kelele za kupinga ushindi wa Trump kwa kudai kuwa huyo sio Rais waliyemchagua, ikumbukwe kuwa mpaka sasa kwa mujibu wa kura zilizopigwa na raia wa Marekani zinaonesha Hillary Clinton anaongoza kwa kupata kura nyingi.

  Sasa sheria za uchaguzi nchini humo zinasema ili mgombea aweze kutangazwa mshindi wa kiti cha Urais inatakiwa pamoja na kura za wananchi ni lazima apate kura za wajumbe 270 au zaidi kati ya wale 538 Wajumbe kutoka Majimbo mbalimbali na ni kitu ambacho Donald Trump amefanikiwa kukipata pamoja na kuwa kura za wananchi zilikua pungufu kwake.

  Baada ya kuwepo maandamo ya siku ya pili mfululizo kumtaka Trump aachie nafasi hiyo, Rais huyo mteule ameandika kwenye Twitter account yake kuwa watu wanaofanya hivyo wanashinikizwa na vyombo vya habari wakati wakijua kuwa yeye ni mshindi halali na hawamtendei haki.

  ‘Nimekua na uchaguzi wenye mafanikio na uwazi, sasa Waandamanaji wanaoshinikizwa na vyombo vya habari wanaandamana, hii sio haki…’ – Trump

  Kwenye Tweet nyingine Trump aliandika jinsi alivyokua na siku nzuri Washington DC walipokutana na Rais Obama kwa mara ya kwanza, kilikua ni kikao kizuri… Melanie (Mke wake) amevutiwa sana na mke wa Rais Obama

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku