Nov 7, 2016

Anayetumia Majina ya Viongozi Kutapeli Aibuka

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kilimanjaro, Wilbroad Mutafungwa amesema jeshi hilo linaendelea kumsaka mtu anayetumia majina ya viongozi wa Serikali kuwatapeli wananchi.

Mutafungwa amewatahadharisha wananchi kuwa makini wanapopigiwa simu kwa namba wasizozijua na kuombwa fedha kwani matapeli nao wanatumia mbinu nyingi.

Mkuu wa mkoa huo, Said Mecky Sadiki amesema alipata ya jina lake kutumiwa na tapeli huyo na tayari  ameishawapa polisi.

“Anabadilisha badilisha namba wameshindwa kumkamata.  Ni zaidi ya mwezi sasa. Kuna wengine hao waliopigiwa simu wameshalipa hela. Mara aseme nina harusi ya mtoto wangu mara sijui nini. Lakini ni kweli huyo mtu yupo,” amesisitiza Sadiki.

Msemaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Innocent Mungy, amesema kusajili laini kwa jina bandia ni kosa la jinai hivyo mmiliki wa namba hiyo pamoja na aliyeisajili anapaswa kushtakiwa kwa jinai.

“Hilo tayari ni kosa la jinai kujifanya mtu ambaye sio na kwa maana hiyo ni police case (shauri la polisi) hivyo aliyejisajili na aliyesajiliwa wana makosa,” amesema.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR