• Breaking News

  Nov 14, 2016

  Bodi ya Mikopo Yawapa Siku 30 Wadaiwa Sugu

  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) imetoa siku 30 kwa wadaiwa sugu kulipa madeni wanayodaiwa vinginevyo watafikishwa mahakamani.

  Akizungumza leo Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi hiyo, Abdul Razaq Badru amesema mbali na kuwafikisha mahakamani kuanzia leo wataanza kutangazwa hadharani kupitia tovuti ya bodi.

  Amesema wadaiwa sugu ni waliokopa na baada ya kumaliza vyuo walipewa miezi 12 ili waanze kurejesha mikopo lakini hawajafanya hivyo.

  "Kukopa harusi kulipa matanga ni lazima hatua zianze kuchukuliwa sasa ili fedha hizo zitumike kuwakopesha wengine"amesema.

  Kwa mujibu wa takwimu za bodi hiyo kuna wadaiwa sugu 142470 ambao wanadaiwa Sh 240 bilioni.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku