• Breaking News

  Nov 16, 2016

  Breaking News:Taarifa Muhimu Kutoka Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania

  Tume ya Vyuo Vikuu Tanzania (TCU) imefunga rasmi utaratibu wa kupokea maombi ya kujiunga na elimu ya juu kwa mwaka wa 2016/17.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu Mtendaji wa tume hiyo kwa vyombo vya habari Dar es Salaam, tayari orodha ya majina ya waliochaguliwa kujiunga na vyuo mbalimbali nchini ilishatangazwa katika vyuo husika.

  “Aidha, wote waliochaguliwa wanaweza kuona vyuo na programu walizochaguliwa kupitia tovuti ya tume ambayo ni www.tcu.go.tz,” ilisema taarifa hiyo.

  Taarifa hiyo ilifafanua kuwa kuanzia sasa mfumo wa pamoja wa udahili (CAS) kwa mwaka wa masomo 2016/17 nao umefungwa rasmi.

  Ilisema waombaji wote waliopangiwa vyuo husika wanatakiwa wawe wameripoti kwenye vyuo husika kwa usajili na taratibu nyingine kabla ya muda wa usajili haujaisha.

  Tume hiyo ilibainisha kuwa kwa wale wanaotaka kuhama vyuo, taratibu zote za kuhama chuo au programu zitafanyika vyuoni na kuthibitishwa na TCU.

  “Mwisho wa kupokea maombi ya uhamisho ni Novemba 18, mwaka huu na hakuna maombi yatakayopokelewa baada ya muda huo,” ilisisitiza taarifa hiyo.

   -HABARILEO

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku