Kaimu Naibu Mkurugenzi wa Habari wa Chama cha Wananchi (CUF), Mbarala Maharagande amemuomba Rais Magufuli kutoisaini sheria ya Huduma ya Vyombo vya Habari iliyopitishwa bungeni juzi

Maharagande amesema sheria hiyo haifai kwa masilahi ya Taifa, wananchi, ustawi wa demokrasia, utawala wa sheria na unabana haki za binadamu.

Amesema hadi muswada huo unapitishwa na Bunge na kuwa sheria, haukuwa na maoni ya wadau wa habari, hakukuwa na matangazo ya kutosha kwa wananchi kupata maoni yao na kuna tatizo la waziri kupewa mamlaka makubwa ya uamuzi.


Post a Comment

 
Top