• Breaking News

  Nov 28, 2016

  FULL LIST: Diamond, Alikiba, Vanessa Mdee, NavyKenzo kwenye Tuzo za SoundCityMVP2016

  Mastaa ambao wako A-List kwenye muziki wa BongoFlava kutoka Tanzania, Diamond Platnumz, NavyKenzo, Vanessa Mde na Alikiba wametajwa kwenye list ya wasanii wanaowania tuzo za SoundCityMVP zinazoandaliw ana kutolewa na kituo cha TV kutoka nchini Nigeria cha Sound City TV.

  Tayari majina na category zote za wasanii watakawania tuzo hizo yametangazwa na kituo hicho na this time kunaonekana kuwa na ushindani mkubwa kwa namna vipengele vilivopangwa. Diamond Platnumz anawania tuzo mbili ikiwemo Msanii Best African Of The Year pia atachuana na mastaa wengine kwenye tuzo ya “Best Male” ambao ni rapa Emtee kutoka South Africa, Wizkid (Nigeria), Patoranking (Nigeria), Falz (Nigeria), Olamide (Nigeria) na Phyno (Nigeria).

  Alikiba anawania tuzo ya Video Bora akicompete na mastaa wengine kama Mr. Eazi – SkinTight, Patoranking – No Kissing, Eddy Kenzo – Mbilo Mbilo, Emtee – Roll Up, DJ Maphorisa – Soweto Baby, Phyno – Fada Fada, Olamide – Who You Epp, Harry Song – Raggae Blues na Mastecraft – Finally.

  Wizkid ndiye ameongozwa kuwania tuzo nyingi zaidi zikiwa ni category 8 zikiwemo nne za number 1 hit single ya ‘Baba Nla’ inayowania tuzo ya Best Song, Best Video, Viewers’ Choice na Listeners’ Choice akifuatiwa na rapa kutoka South Africa, Emtee na Olamide. Soundcity MVP2016 zitatolewa na kuoneshwa Live Alhamisi, 29 December kutoka ndani ya ukumbi wa Expo Center of the Eko Hotel & Suites, Jijini Lagos Nigeria.


  Baada ya kitambo cha kutotajwa kwenye tuzo yoyote hatimaye mwimbaji Davido ametajwa kwenye kipengele cha Digital Artiste of the Year akiwa na Tekno, A.K.A, P-Square, Tiwa Savage, Wizkid na Casper Nyovest. Warembo kutoka East Africa Victoria Kimani (Kenya), na Vanessa Mdee (Tanzania) watachuana kwenye category ya Female MVP of The Year wakiwa na msanii kutoka Ghana, MzVee.

  Wakati Navyo Kenzo wakiwania tuzo ya Best Grouo or Duo wakiwa na Sauti Sol (Kenya), Mafikizolo (South Africa), Micasa (South Africa), R2Bees (Ghana), Toofan (Togo), P-Square – Nigeria na VVIP (Ghana).

  Mwisho wa kupiga kura kwenye tuzo za Soundcity MVP ni tarehe 27 December 2016 au ingia hapa www.soundcitymvp.com.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku