• Breaking News

  Nov 18, 2016

  GEITA: Diwani Asiyejua Kusoma Wala Kuandika Asimamishwa Baada ya Kutohudhuria Vikao Tangu Disemba

  Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita limemsimamisha Diwani wa Kata ya Senga Joel Ntinginya kutoendelea na nafasi yake baada ya kutohudhulia vikao vya baraza tangu kuapishwa kwake Disemba mwaka jana.

  Diwani huyo amekuwa akituhumiwa kutokujua kusoma wala kuandika.

  Baada ya kupoteza sifa ya kuendelea kuwa Diwani wa Kata ya Senga, mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita amesema tayari ameshapeleka barua TAMISEMI kwa ajili ya hatua zaidi.

  1 comment:

  1. Nilimuona wakati anaapishwa na nilisema kwamba hatuwezi kupata maendeleo wa kuchagua viongozi wa aina hiyo, ref: facebook/umwuzukuru wa Maguge

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku