• Breaking News

  Nov 16, 2016

  Haya Hapa Majina ya Watu Maarufu na Vigogo Ambayo ni Miongoni mwa Wadaiwa Sugu wa Bodi ya Mikopo

  Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) jana alichapisha hadharini majina ya wadaiwa sugu walionufaika na mikopo wakiwa vyuoni lakini hadi leo hawajaresha mikopo hiyo.

  Majina hayo yameanzia kwa wanafunzi waliomaliza chuo mwaka 1994/95 huku majina ya watu maarufu na watoto wa vigogo wenye uwezo mkubwa wa kifedha nayo yakiwamo miongoni mwa wadaiwa sugu.

  Miongoni mwa majina ya watu maarufu waliokuwamo katika orodha hiyo iliyochapishwa na gazeti la TanzaniaDaima ni pamoja na Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), Mwesigwa Selestine (1996/97), aliyekuwa Katibu Mkuu wa TFF, Fredrick Mwakalebela, Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Uenezi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), John Mrema, Meya wa Ubungo (CHADEMA), Boniface Jacob.

  Jerry Muro ambaye ni Afisa Habari wa Yanga naye yumo katika orodha hiyo, Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano na Uhamasishaji Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii (SSRA), Sarah Kibonde na Mwanasheria maarufu Majura Magafu.

  Pia mtoto aliyekuwa Waziri Mkuu wa Tanzania na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CHADEMA, Adda E. Lowassa (2006/07) naye ni miongoni mwa wadaiwa sugu waliotajwa.

  Aidha, kuna baadhi ya majina ambayo yamedaiwa ni ya watoto wa vigogo, lakini haijathibitishwa kama ni watoto wao au ni majina yamefanana. Miongoni mwa majina hayo ni Lowassa, Godson Ngoya (2005/06) ambaye anadaiwa kuwa ni mtoto wa Edward Ngoyai Lowassa na Pombe, Ruth John (2009/10) ambaye anadaiwa kuwa ni mtoto wa Rais Dkt John Pombe Magufuli.

  Bodi ya mikopo ya elimu ya juu ilitangaza kuwa inatoa siku 30 kwa wadaiwa sugu wote kurejesha mikopo yao kinyume na hapo watafikishwa mahakamani. Aidha, mbali na kufikishwa mahakamani wadaiwa sugu wote watatakiwa kulipa gharama zilizotumiwa na mamlaka hiyo kuwatafuta.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku