• Breaking News

  Nov 17, 2016

  Jeshi la Polisi Arusha Wadharau Amri ya Mahakama Kupitia Kwa Hakimu Rwezile..Kesi ya Mbunge Godbless Lema

  Nje ya mahakama Arusha kesi ya Lema
  Jana baada kusikilizwa kesi ya Mbunge Lema.
  Arusha. Wakati askari polisi saba watatoa ushahidi mahakamani katika kesi ya uchochezi inayomkabili Mbunge wa Arusha Mjini (Chadema), Godbless Lema, Mahakama imetoa onyo kwa askari Polisi na Magereza wanaowasumbua waandishi wa habari na wananchi.

  Onyo hilo lilitolewa na Hakimu Mkazi Mfawidhi wa Mahakama ya Mkoa wa Arusha, Augustino Rwezile baada ya askari Magereza wakiwa na silaha kuwafukuza waandishi wa habari waliotaka kuchukua kumbukumbu za Lema kufikishwa mahakamani.

  Pia, aliwaonya Polisi ambao wamekuwa wakilalamikiwa kwa kuwazuia wananchi wanapokwenda kusikiliza kesi ya mbunge huyo.


  Leo Alhamisi kuanzia majira ya saa mbili asubuhi Jeshi la Polisi wamezuia wananchi pamoja na waandishi wa habari kuingia ndani eneo la mahakama kufutilia kesi ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema.

  My take: Jeshi la Polisi wanatoa wapi mamlaka ya kudharau Amri ya Mahakama kupitia Hakimu Rwezile?

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku