• Breaking News

  Nov 3, 2016

  Joh Makini Amewachana Wanamuziki Wanaoanzisha Label


  Rapa mkali kutoka Weusi Joh Makini amewachana wanaoanzisha label hapa nchini kuwa wengi wao hawajui vigezo vya kumiliki label na badala yake wanazitumia label kama kiki katika muziki wao


  Akipiga story ndani ya eNewz amesema Weusi wana mipango mingi ikiwemo kuanzisha label yao japo wana baadhi ya vijana wanaowasaidia lakini hawawezi kujitangaza kuwa ni label ya kusaidia wasanii kwa kuwa msaada wanaoutoa ni wa kawaida na sio wakutangaza mitandao.


  Hata hivyo Joh hakusita kuelezea mahusiano ya weusi na Lord Eyez kuwa “Lord hajatengwa na bado ni mmoja wa wanafamilia katika kundi letu la Weusi kuna wimbo wa Lord tulikuwa studio tukiuandaa juzi japo watu wanaongea mengi kuhusu ukaribu wetu na Lord kwa sasa ila siyo mbaya wakituzungumzia kwa kuwa ni sehemu ya maisha yetu” alisema Joh.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku