• Breaking News

  Nov 2, 2016

  Kaduguda: Manji na Dewji Wasidhani Pesa Itasaidia Kuuokoa Mpira Nchini

  Aliyewahi kuwa Katibu Mkuu wa FAT na klabu ya Simba, Mwina Kaduguda amewaambia matajiri wa Simba na Yanga akiwemo Yusuph Manji na Mohammed Dewji kuwa wasidhani kuwa pesa inaweza ikamaliza matatizo ya mpira nchini.

  Akiongea na kipindi cha Sports HQ ya EFM, Kaduguda amesema kuwa pesa haiwezi kusaidia mpira wa Tanzania kwa kuwa kwenye shirikisho la TFF kuna viongozi ambao hawana sifa za kukaa kwenye nafasi hizo.

  “Napenda kuwaambia Manji na Dewji kuwa pesa haiwezi ikauokoa mpira wa Tanzania, wao wanajua kuwa pesa inaweza ikamaliza kila kitu. Angalia Abrahamovic pale Chelsea anaimiliki timu lakini kawaachia viongozi ambao wanaiendesha,” amesema Kaduguda.

  “Tukubali tukatae TFF kuna viongozi hawana sifa za kuwepo pale lakini ukionekana kiongozi mzuri wanakupinga. Nina uhakika kama Manji angeweza kuangalia zaidi kwenye uongozi kuliko kwenye pesa, leo hii timu hiyo ingecheza nusu fainali au mpaka fainali ya kombe la Shirikisho Afrika.”

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku