• Breaking News

  Nov 7, 2016

  Kikwete Asema Tanzania itaandikwa Kwa Wino wa Dhahabu Kupitia Michezo

  Rais mstaafu wa awamu ya nne, Jakaya Mrisho Kikwete, amesema muda si mrefu Tanzania itaandikwa na wino wa dhahabu kwenye sekta ya michezo na kuja kuitangaza Tanzania kimataifa.

  Kikwete ameyasema hayo wiki hii katika fainali za mpira wa kikapu kwa vijana zilizofanyika katika Kituo cha Vijana cha Michezo cha Jakaya Kikwete,kilichopo jijini Dar es Salaam.

  “Uwekezaji wa watoto wadogo kimichezo ni vizuri sababu unainua vipaji vya watoto na hatimaye kupata wachezaji wazuri hapo baadae kama wa mpira wa miguu, kikapu na wa pete. Kituo hiki kimefundisha zaidi ya watoto elfu 50,” alisema.

  “Wakiwekeza hapa Tanzania itaandikwa kwa wino wa dhahabu miaka ijayo kupitia michezo ambao wachezaji wake watatoka katika kituo hiki.”

  BY: EMMY MWAIPOPO

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku