Nov 17, 2016

Kocha Mpya wa Yanga Kusajili Wachezaji Wawili

George Lwandamina
Kocha mpya wa Yanga Mazambia George Lwandamina baada ya kusaini mkataba wa miaka miwili ameanza kukifumua kikosi hicho baada ya kupendekeza jina la mshambuliaji wa kimataifa wa Kenya Jesse Were asajiliwe kipindi hiki cha dirisha dogo.

Katibu mkuu wa Yanga Baraka Desidedit, aliuambia mtandao wa Goal, kwamba kocha wao mpya Lwandamina anataka kusajili nyota wawili wapya kutoka klabu ya Zesco aliyokuwa akiifundisha kabla ya kutua Yanga mmoja wapo akiwa Were anayecheza nafasi ya ushambuliaji na kiungo mkabaji Meshack Chaila ambaye jina lake ndiyo lilikuwa la kwanza kupendezwa na kocha huyo.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR