• Breaking News

  Nov 16, 2016

  Lowassa Afafanua Kutoonekana Kwake Misibani

  Waziri Mkuu wa zamani, Edward Lowassa ametoa ufafanuzi kuhusu kutoonekana kwake kwenye misiba ya viongozi wawili wa zamani serikalini, Samuel Sitta na Joseph Mungai.

  Sitta, aliyekuwa Spika wa Bunge la Tisa, alifariki dunia Novemba 7, akiwa Ujerumani alikokwenda kutibiwa tezi dume na siku iliyofuata alifariki Mungai, aliyekuwa Waziri wa Elimu wa Serikali ya Awamu ya Tatu.

  Gumzo kwenye mitandao ya kijamii lilikuwa ni kutoonekana kwa Lowassa, ambaye hivi sasa ni mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema.

  Lowassa aliliambia gazeti hili jana kuwa, kilichomkwamisha kufika kwenye misiba hiyo ni kuwa safarini Afrika Kusini alikokwenda kumuangalia mdogo wake, Bahati Lowassa aliyekuwa mgonjwa.

  2 comments:

  1. Maelezo hayo ya Lowassa hayajitoshelezi mtu kama huyo mwenye uwezo wa kuchukua hata ndege binafsi akawahi mazishi na kurudi tena south. Hapa napata shida kabisa kuelewa there must be another reasons. Awe open tu kwa wananchi. Hasa sisi CHADEMA

   ReplyDelete
  2. Maelezo hayo ya Lowassa hayajitoshelezi mtu kama huyo mwenye uwezo wa kuchukua hata ndege binafsi akawahi mazishi na kurudi tena south. Hapa napata shida kabisa kuelewa there must be another reasons. Awe open tu kwa wananchi. Hasa sisi CHADEMA

   ReplyDelete

  Siasa

  Michezo

  Udaku