Nov 26, 2016

Machinga Mwanza 'Wamtunishia Misuli' Mkuu wa Wilaya

Wafanyabiashara ndogondogo  (machinga) Jijini Mwanza wamefanya mkutano asubuhi ya leo lengo kubwa likiwa ni kuipinga kauli ya mkuu wa wilaya ya Nyamagana Marry Tesha  yakuwataka waondoke ndani ya siku 7.

Akizungumza katika mkutano huo mwenyekiti wa machinga Said Tembo amesema wao kama machinga wako tayari kwa lolote hata kama ataanza leo oparesheni yake atawakuta wapo katika maeneo yao ya biashara na hakuna mtu yeyote atakayeondoka katika eneo la biashara.
Mwenyekiti huyo amesema wao kama wafanyabiashara wanasimamia kauli ya Rais aliyoitoa juu ya machinga kutokuondolewa mjini badala yake watengewe maeneo mengine ambayo yako katikati ya mji na si nje ya mji kama alivyofanya mkuu huyo na  kuongeza kuwa Raisi akitoa kauli siku zote kauli hiyo huwa sheria.

Moja kati ya machinga akizungumza katika mkutano wao
hata hivyo machinga hao wamesema hawako tayari kuondoka kwa sababu hakuna makubaliano yoyote yaliyofanyika  kati yao na serikali ili kufikia muafaka wa jambo hilo hivyo wanaisubiri siku hiyo ifike ili wajue mwanzo na mwisho wao.

Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR