• Breaking News

  Nov 18, 2016

  Magufuli Akosa Tuzo ya Forbes Person of The Year 2016, Yaenda Kwa Mwanasheria wa Afrika Kusini

  Usiku wa Alhamisi ya Novemba, 17 kumefanyika halfa ya utoaji wa tuzo ya Forbes Person Of the Year kwa mwaka 2016 ambazo zilikuwa zikiwashirikisha watu watano kutoka mataifa mbalimbali Afrika.

  Mmoja wa washirki wa tuzo hizo alikuwa ni Rais wa Tanzania, Dkt. John Magufuli ambaye alikuwa akishindana na Michiel Le Roux – mwanzilishi wa benki ya Capitec ya Afrika Kusini, Thuli Madonsela – mwanasheria na mtetezi wa haki za binadamu wa Afrika Kusini, Rais wa Mauritian, Ameenah Gurib na watu wa Rwanda.

  Katika halfa ya utoaji wa tuzo hizo, Mwanasheria na mtetezi wa jamii wa Afrika Kusini, Thuli Madonsela ametajwa kuwa mshindi wa Tuzo ya Forbes Person of the Year 2016 kutokana na juhudi zake anazozifanya za kusaidia jamii ya watu wa Afrika Kusini katika mambo mbalimbali yakiwepo ya kisheria.

  Thuli Madonsela anakuwa mshindi wa sita wa tuzo hizo tangu zianzishwe mwaka 2011, washindi waliopita walikuwa ni Sanusi Lamido Sanusi – 2011, James Mwangi – 2012, Akinwumi Adesina – 2013, Aliko Dangote – 2014 na Mohammed Dewji – 2015.

  Kwa kushindwa huko kwa Rais Magufuli, Mohammed Dewji ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji na Rais wa Makampuni ya Mohammed Enterprises Tanzania Limited (MeTL Group) anasalia kuwa Mtanzania pekee ambaye amewahi kushinda tuzo hiyo

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku