• Breaking News

  Nov 25, 2016

  Mahakama Yaamuru Yusuf Manji Aondoke, Awalipe


  MAHAKAMA Kuu, Divisheni ya Ardhi, jijini Dar es Salaam, imeamuru Kampuni ya Quality Group inayomilikiwa na mfanyabishara Yusuph Manji na wenzake kuondoka kwenye jengo la Quality Plaza na kulipa kodi ya pango wanayodaiwa tangu mwaka 2007 mpaka sasa.


  Fedha hizo zitalipwa kwa mlalamikiwa wa kwanza kwenye kesi hiyo, Kampuni ya Image Properties and Estate ambayo ni wakala wa Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF), unaomiliki jengo hilo.

  Uamuzi huo ulitolewa jana na Msajili wa Mahakama hiyo, Frank Mahimbali, kwa niaba ya Jaji John Mgetta katika kesi nne zilizofunguliwa na Kampuni ya Quality Group kupinga kulipa kodi ya jengo hilo.

  Kesi hizo zilitokana na mdai Quality Group kukimbilia Mahakamani kufungua shauri jipya kila alipokuwa akipelekewa notisi ya kuhama katika jengo hilo na mlalamikiwa wake, Kampuni ya Image Properties and Estate.

  Source: Nipashe

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku