• Breaking News

  Nov 18, 2016

  Majibu ya Bodi ya Mikopo Kuhusu Wadaiwa Sugu Waliofariki


  Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Juu (HESLB) imetoa ufafanuzi kuhusu watu wanaodaiwa na bodi hiyo ambao tayari walikwishapoteza maisha, ambapo imesema kuwa itawafuatilia wadhamini wao ili walipe kwa niaba yao.


  Akizungumza katika kipindi cha EA Breakfast kinachoruka kupitia East Africa Radio, Mkurugenzi Mtendaji wa bodi hiyo Abdul-Razaq Badru amesema kuwa suala la kukusanya madeni hayo ni la kisheria hivyo bila kujali kama mdaiwa amepofariki, lazima uwepo utaratibu wa kurejesha mikopo hiyo kupitia kwa ndugu, jamaa na wadhamini wa muhusika.


  Amelazimika kutoa ufafanuzi huo kutokana na kuwepo kwa majina ya watu ambao wamefariki katika orodha ya wadaiwa sugu iliyotolewa na bodi hiyo hivi karibuni.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku