• Breaking News

  Nov 18, 2016

  Makonda Aibua Maswali Kwa Kauli yake

  Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda juzi alishusha tuhuma nzito dhidi ya wajumbe wake wa Kamati ya Usalama ya Mkoa, huku akiacha maswali kuhusu utendaji na mchango wake katika kufanikisha mkakati wa Serikali kupambana na rushwa.

  Kwa cheo chake cha ukuu wa mkoa, Makonda ni mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa ambayo kipolisi Dar es Salaam ni kanda ikiwa na mikoa mitatu ya kipolisi; Kinondoni, Ilala na Temeke.

   Akizungumza kwenye hafla ya uzinduzi wa kituo cha uboreshaji huduma za umeme juzi, Makonda alisema kuna kikundi cha watu kumi wanaojishughulisha na biashara ya kilevi cha shisha ambacho kilienda ofisini kwake kumshawishi awaruhusu waendelee na biashara hiyo na kwamba kila mwezi wangempa Sh5 milioni kila mmoja.


  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku