• Breaking News

  Nov 7, 2016

  Makonda Kujenga Vituo vya Polisi vya Kisasa Dar es salaam

  Mkuu wa mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda amesema kuwa ana mpango wa kujenga vituo vya polisi vya kisasa katika mkoa wake.

  Ametoa kauli hiyo katika ziara yake ya kukagua vituo vya polisi vilivyopo jijini humo na kuongeza kuwa serikali inampango wa kuongeza vituo vya polisi vya kisasa kwa lengo la kuimarisha hali ya ulinzi na usalama mkoani humo.

  “Kumekuwa na malalamiko ya vituo vya polisi vinafungwa mapema, kumekuwa na malalamiko kwa wananchi kupiga simu polisi kuomba msaada hakuna polisi anaejitokeza,nikaona kuna sababu ya kuangalia vituo vyetu vikoje,alisema Makonda.

  “Binadamu siku zote kabla hujamuukumu mwenzako lazima uangalie mazingira aliyonayo pia waswahili wanakwambia vaa kiatu chake kwanza alafu ndo umseme vibaya. Agenda tuliyonayo sisi ni moja ni kujenga vituo vikubwa vyenye uwezo wakuwahudumia wananchi wote wakati wote wa masaa 24 hiyo ndo agenda ambayo ninayo,”aliongeza.

  Mkuu wa mkoa huyo pia ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama mkoa wa Dar es salaam.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku