Nov 20, 2016

Mali za Walioshiriki Kufilisi Benki ya Twiga zaanza Kukamatwa


Hatimaye Benki kuu Tanzania inayoisimamia Benki ya Twiga imeanza zoezi lakukamata mali za wafanyabishara na wadaiwa sugu walioshiriki kufilisi Benki ya Twiga na kutoa wiki moja kwa wadaiwa kulipa mikopo ili kunusuri mali zao kuuzwa kwa mnada.

ITV imeshuhudia maduka ya vifaa vya ujenzi katika maeneo mbalimbali ya Kariakoo na,tabata yakifungwa kwa makufuli na kuzungushia utepe unaozuia kufunguliwa,ambapo akizungumza na waandishi wa habari kiongozi wa timu inayofanya zoezi hilo bwana Richard Nkanyemka amesema Benki ya Twiga inadai wafanyabiashara zaidi ya shilingi bilioni 8 na kuwataka kulipa fedha hizo ili kunusuru biashara zao kupigwa mnada.

Kwa upande wao baadhi ya wenyekiti wa serikali ya mtaa wamekiri kupata taarifa ya kufanyika kwa zoezi la kukamata mali za wafanyabiashara hao, ambao wamesema kutokana na ugumu wa maisha zoezi la kupigwa mnada nyumba za watu pamoja na biashara kutokana na mikopo ya benki imezidi kuongezeka kutokana na wadaiwa kushindwa kulipa mikopo yao.


Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR