BUNGENI: Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe amedai Wabunge wa CCM wamehongwa Shilingi Milioni 10 kila mmoja ili wasaidie kupitisha Muswada wa Habari.

Mbowe amesema kikao hicho kilifanyika mnamo tarehe 25/10/2016 saa mbili usiku na kiliongozwa na Waziri Mkuu akiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahaman Kinana.

Mbowe aliyasema hayo akimuuliza swali la papo kwa hapo Waziri Mkuu, hata hivyo swali hilo lilikataliwa na Naibu Spika kwa madai kuwa sio la Kisera.


Post a Comment

 
Top