• Breaking News

  Nov 15, 2016

  Mbunge Chadema Ajipanga Kuonana na Magufuli

  Mbunge wa Moshi Mjini, Jaffar Michael (Chadema), anatafuta fursa ya kuonana na Rais John Magufuli ili aingilie kati kukwama kwa mradi wa ujenzi wa kituo kipya cha kisasa cha mabasi katika Manispaa ya Moshi.Tokeo la picha la magufuli

  Kituo hicho kitakachokuwa na majengo ya ghorofa na cha kwanza cha aina yake Afrika Mashariki na Kati, kimepangwa kujengwa eneo la Ngangamfumuni kwa gharama ya zaidi ya Sh20 bilioni.

  Mbunge huyo amemlaumu Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (Tamisemi), George Simbachawene akidai anachelewesha kutoa idhini ya kuanza ujenzi wa mradi huo.

  No comments:

  Post a Comment

  Siasa

  Michezo

  Udaku