Nov 1, 2016

Mbunge Lema Anusurika Kutekwa, Aokolewa na Polisi

Mbunge wa Jimbo la Arusha Godbless Lema usiku wa kuamkia leo,  amenusurika kutekwa na Majambazi eneo Makuyuni Wilayani Monduli akitokea Bungeni Dodoma.

Akisimulia tukio hilo, amesema alitoka Dodoma saa moja  usiku na kufika Makuyuni saa saba usiku wa kuamkia leo, ndipo mita hamsini kutoka kizuizi cha Polisi, alikuta mawe makubwa barabarani na malori mawili yamesimama, akagundua ni majambazi na kuamuru dereva kugeuza gari lake.

Amesema alikuwa katika gari namba T.114 DGR Land Cruser V8, ambalo waliona watu zaidi ya kumi wakitoka pembeni ya barabara wakiwa na marungu na mapanga wakiturushia mawe, lakini tulifanikiwa kukimbia na kutoa taarifa Polisi, ambao walifanikiwa kumuua Jambazi mmoja.

Kamanda wa Polisi, Charles Mkumbo amekiri kutokea kwa tukio hilo na kudai wamepata taarifa kwa raia wema ambapo Polisi wa doria waliwahi kufika eneo la tukio na kufanikiwa kumuua jambazi mmoja ambaye jina lake halijafahamika mara moja katika majibizano  ya risasi na Polisi.


Amesema jambazi huyo akiwa na wenzake 29 wakiwa na bunduki ambayo aina yake haijajulikana na silaha za jadi,, huku wakiwa wameweka mawe barabarani,walisimamisha gari aina ya fuso lenye namba T.871 BUZ lililokuwa likitoka Moshi kwenda Singida likiwa na mzigo mzito na kumpora abiria mmoja Victor Pius (46) Mfanyabiashara, Mkazi wa Majengo Mosho.

Pia abiria huyo aliporwa simu mbili  aina ya Nokia na Samsung na fedha tasilimu shlingi 50,000.
Amesema pia wamefanikiwa katika tukio hilo kukamata majambazi 12 papo hapo wakiwa na mapanga sita na marungu manne.Bonyeza HAPA Kudownload Application ya Udaku Special Blog Kwenye Simu Yako

Share:

0 maoni:

Post a Comment

Trending News

Copyright © Siasa Huru | Powered by Blogger Design by JK | Blogger Theme by JR